Courtois azua makuhwa Chelsea, akutana na kocha Sarri - Darajani 1905

Courtois azua makuhwa Chelsea, akutana na kocha Sarri

Share This

Licha ya kocha Maurizio Sarri kusema anategemea majibu mazuri kutoka kwa nyota wake ambao wamekuwa wakihusishwa kuondoka Chelsea akiwemo mlinda mlango, Thibaut Courtois lakini imekuwa tofauti mara baada ya kuripotiwa kwamba kipa huyo amemwambia kocha Sarri kwamba anataka kuondoka.

Chanzo cha ESPN kimedai kwamba mlinda mlango huyo amemwambia kocha Sarri kwamba hatazimii kuendelea kubaki Chelsea na badala yake anataka kuondoka.

Mlinda mlango huyo mwenye miaka 25 amebakiza mkataba wa mwaka mmoja klabuni Chelsea na kama ikishindikana kumshawishi akasajni mkataba mpya basi ataondoka bure kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment