Kante akubali kufunga pingu kusalia Darajani - Darajani 1905

Kante akubali kufunga pingu kusalia Darajani

Share This

Nyota wa Chelsea, N'Golo Kante anatajwa na chanzo kimoja cha habari cha nchini kwao, Ufaransa kwamba amekubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Chelsea.

Nyota huyo ambaye aliiongoza vyema timu yake ya taifa ya Ufaransa kushinda taji la Kombe la Dunia mwezi uliopita anatajwa kukataa ofa za kujiunga na klabu za PSG na Barcelona zilizokuwa zikitajwa kumfukuzia na badala yake amekubali kusalia klabuni Chelsea.

Aliwasili klabuni hapo mwaka 2016 akitokea Leicester city na kufanikiwa kufanya vyema mpaka kushinda tunzo kadhaa ikiwemo tunzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2016-2017 akiisaidia vyema Chelsea kushinda taji la ligi kuu Uingereza.

Mkataba wake wasasa unamalizika mwaka 2021.

No comments:

Post a Comment