Martial kutua Chelsea ili kuziba pengo - Darajani 1905

Martial kutua Chelsea ili kuziba pengo

Share This

Klabu ya Chelsea inahofia kumpoteza winga wake, Eden Hazard ambaye anatajwa na vyombo vingi vya habari kwamba anakaribia kutua klabuni Real Madrid akiwemo mchezaji wa zamani wa Chelsea, Gus Poyet ambaye anaamini mchezaji huyo hataki kubaki Chelsea.

Wasiwasi wa kuondoka kwa nyota huyo kumeifanya klabu hiyo kuanza taratibu za kumfukuzia winga nyota wa klabu ya Manchester united, Anthony Martial ambaye anatajwa kutaka kuachana na klabu hiyo.

Chelsea inatajwa pia kumfukuzia nyota wa Olympique Lyon, Nabil Fekir ili azibe pengo la Hazard endapo nyota huyo ataondoka.

No comments:

Post a Comment