M/Kirafiki; Habari muhimu kuelekea mchezo Perth Glory vs Chelsea - Darajani 1905

M/Kirafiki; Habari muhimu kuelekea mchezo Perth Glory vs Chelsea

Share This

Klabu ya Chelsea ipo nchini Australia kwasasa ikienda huko kwa lengo la kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kati ya klabu hiyo dhidi ya wenyeji wa jiji la Perth nchini humo, klabu ya Perth Glory ambayo kwasasa ipo chini ya kocha msaidizi wa zamani wa Crystal Palace, Popovic huku kocha Maurizio Sarri wa Chelsea akishuka kwenye mchezo huo siku 9 toka atambulishwe kuwa kocha mpya wa Chelsea akichukua mikoba ya kocha Antonio Conte.

Kuelekea kwenye mchezo huo hapa nakuletea habari muhimu unazotakiwa kuzijua kuhusu mchezo huo.

Kuhusu mchezo
Mchezo huu ni maalumu kwa ajili ya kuuzindua uwanja wa kisasa uliopo nchini humo unaojulikana kama Optus Stadium huku timu hizo zikiwa timu za kwanza za soka kucheza kwenye uwanja huo.

Chelsea
Kocha Maurizio Sarri amechagua wachezaji 25 ambao hawakushiriki kwenye michuano ya Kombe la Dunia na hivyo kumaanisha Chelsea itacheza ikiwakosa nyota wake 14 ambao walishiriki michuano hiyo wakiweno Eden Hazard, N'Golo Kante na Thibaut Courtois.

Kikosi kinachodhaniwa kuanza siku hiyo; Marcin Bulka, Thomas Kalas, David Luiz, Davide Zappacosta, Marcos Alonso, Tiemoue Bakayoko, Cesc Fabregas, Jorginho, Alvaro Morata, Tammy Abraham, Pedro (4-3-3)

Perth Glory
Huu ni mchezo wa kwanza kwa kocha mpya wa klabu hiyo Popovic ambaye alishawai kuwa kocha msaidizi kwa klabu ya Crystal Palace ya nchini Uingereza huku akiifundisha klabu hiyo ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya nane katika msimamo wa ligi kuu yenye timu kumi ya nchini humo.

Historia
Mara ya mwisho kwa Chelsea kucheza mchezo wake nchini Australia ilikuwa ni mwaka kipindi cha kocha mreno, Jose Mourinho ambaye aliondoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Sydney ya nchini humo. Loic Remy akiwa mfungaji.

Tarehe; 23-Julai-2018
Muda; Saa 2:30 Mchana (Saa 14:30) kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment