Morata yupo njiani kuelekea Italia - Darajani 1905

Morata yupo njiani kuelekea Italia

Share This
Tarehe kama ya leo mwaka jana klabu ya Chelsea ilifanikiwa kumnasa mshambuliaji raia wa Hispania, Alvaro Morata kutoka klabu ya Real Madrid kwa dau lililomfanya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi klabuni Chelsea.
Lakini toka nyota huyo akamilishe usajili huo wa kutua klabuni Chelsea amekuwa akiripotiwa mara kadhaa kutamani kurejea nchini Italia ambapo huko alifanya mengi makubwa akiwa na klabu ya Juventus na nia yake hiyo ya kurejea Serie A imekuwa ikitajwa sana wakati msimu uliopita ulipokuwa ukielekea mwishoni ambapo alikuwa na kasi ndogo katika ufungaji fofauti na alivyoanza msimu ambapo kwenye michezo nane ya mwanzoni alifanikiwa kufunga magoli nane.
Inataarifiwa kwamba ukame wake aliomalizia msimu umemfanya mchezaji wa zamani wa klabu ya AC Milan, Luca Antonini kuamini nyota huyo yupo njiani kuelekea nchini Italia ambapo huko anatakiwa na klabu hiyo ya AC Milan.
Antonini alikiambia chombo cha habari cha RMC Sport kwamba anaamini nyota huyo ameshafanya makubaliano na klabu hiyo ya AC Milan na akiamini nyota huyo mwenye miaka 25 yupo njiani kutimkia AC Milan na atajiunga na klabu hiyo katika dirisha hili kubwa la usajili.

No comments:

Post a Comment