Huyu ndiye kocha Maurizio Sarri - Darajani 1905

Huyu ndiye kocha Maurizio Sarri

Share This

Jana ilikuwa ni siku ya kumbukumbu kwa nyota wa zamani ambaye ni gwiji wa Chelsea, Didier Drogba ambapo alisajiliwa na Chelsea tarehe na mwezi kama wa siku ya jana mwaka 2004 na hata leo pia ni siku ya kumbukumbu ya wiki moja.

Ndiyo wiki moja. Siku kama ya leo namaanisha jumamosi iliyopita klabu ya Chelsea ilimtangaza kocha Maurizio Sarri kuwa ni kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya kocha Antonio Conte.

Leo nataka nikupe kidogo jambo au mambo ambayo labda huyafahamu kuhusu kocha huyu raia wa Italia.

Mwezi Januari mwaka 1959 ndiyo ilikiwa siku na mwaka ambao kocha huyu mwenye sifa ya kuvuta sana sigara alizaliwa huko jijini Naples nchini Italia.

Tukiachana na mambo mengi yaliyotokea hapo kati je unajua kama kocha huyu hakuwai kucheza soka la kulipwa? ndo hivyo hakuwai kucheza lile soka la kitaaluma na badala yake alikuwa akicheza soka la mtaani na la kistarehe. Yani hakucheza kwenye ngazi kubwa.

Na unajua kama kocha huyo alikuwa mfanyakazi wa benki? eeh yani alikuwa akifanya kazi benki mida ya asubuhi kisha mchana na jioni alikuwa akicheza mpira kwenye klabu za mtaani. Kufanya kazi kwake benki kulimfanya asafiri kwenye majiji mbalimbali ikiwemo jiji la London nchini Uingereza ambapo kwasasa anafanya kazi jijini hapo akiwa kama kocha wa Chelsea.

Jambo jengine unajua kama Maurizio Sarri ni moja ya makocha waliofundisha klabu nyingi barani Ulaya. Alianza kazi ya ukocha mwaka 1990 na mpaka kufikia Chelsea ameshazifundisha klabu 19 lakini akitamba haswa na klabu za Empoli na Napoli zote za Italia.

Ni hayo tu kwa leo...

No comments:

Post a Comment