Chelsea yatua kwa Pepe Reina - Darajani 1905

Chelsea yatua kwa Pepe Reina

Share This

Hii ni tetesi iliyoripotiwa na gazeti moja la nchini Italia, Premium Sport ambalo limetoa ripoti kwamba klabu ya Chelsea inamfukuzia mlinda mlango mpya wa klabu ya AC Milan, Pepe Reina.

Mlinda mlango huyo mwenye miaka 35 anatajwa kutakiwa na kocha wake wa zamani klabuni Napoli, Maurizio Sarri ambaye kwasasa ni kocha wa Chelsea na inaelezwa kocha huyo anataka kuungana na mlinda mlango huyo raia wa Hispania ambaye waliwai kufanya kazi pamoja klabuni Napoli.

Reina ambaye aliwai kuichezea klabu ya Liverpool amejiunga na klabu ya AC Milan ambayo amejiunga nayo kwa mkataba wa miaka mitatu lakini bado tetesi za kutakiwa na Chelsea zimeripotiwa.

No comments:

Post a Comment