Klabu ya Chelsea imekuwa ikitajwa kumfukuzia nyota na kiungo wa klabu ya CSKA Moscow, Aleksandr Golovin huku usajili huo ukiwa unachelewa kutimia kila inadhaniwa usajili huo kukamilika
Klabu ya As Monaco ndiyo inaonekana kuwa kikwazo kikubwa katika usajili huu wa nyota raia wa Urusi.
Rais wa klabu ya CSKA Moscow alikaririwa akisema kiongozi mmoja wa klabu ya AS Monaco alifika klabuni kwao na kuonyesha nia ya kumtaka nyota huyo.
Lakini kuna taarifa nzuri kutoka kwa mlinda mlango wa zamani wa CSKA Moscow, Sergei Andreyevich Chepchugov ambaye aliutumia mtandao wa Instagram akituma ujumbe wa kumtakia heri nyota huyo akisema miaka miwili iliyopita niliwai kukwambia baada ya muda utakuwa nyota kwenye klabu kubwa barani Ulaya na nakutakia maisha mema huku akimalizia kwa kuandika #Chelsea na kuonekana kwamba nyota huyo yupo mbioni kujiunga na Chelsea.
Huenda ujumbe huu ukafufua tumaini jipya kwa mashabiki na klabu ya Chelsea ambayo ilikuwa na hofu ya kumkosa nyota huyo mara baada ya kuripotiwa kwamba klabu ya As Monaco imetoa dau la paundi milioni 35.
No comments:
Post a Comment