Kuelekea mchezo wa nchini Australia, je unalijua hili? - Darajani 1905

Kuelekea mchezo wa nchini Australia, je unalijua hili?

Share This

Klabu ya Chelsea itacheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Perth Glory siku ya jumatatu ya tarehe 23-Julai katika uwanja wa Optus huko nchini Australia.

Lakini je unalijua hili kuhusu mchezo huo? unajua kama mlinda mlango wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Australia, Mark Schwazer ndiye aliyekuwa balozi wa kuuandaa mchezo huo.

Eeh ndio hivyo, mchezo huu utakaochezwa saa 14:30 kwa saa za Afrika Mashariki uliandaliwa maalumu kwa lengo la kuufungua uwanja mpya wa Optus Stadium ambao unapatikana jijini Perth huko Magharibi mwa nchi hiyo ya Australia huku mkongwe huyo akitumika kama balozi au mwakilishi wa Chelsea siku hiyo.

No comments:

Post a Comment