Inaripotiwa kwamba kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri amemfanya mshambuliaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Argentina, Gonzalo Higuain kuwa ni mchezaji chaguo lake la kwanza anayetaka kumsajili katika dirisha hili kubwa la usajili ambalo linamalizika mwezi Agosti mwaka huu.
Huku ikizidi kuripotiwa kwamba kocha huyo mwenye miaka 59 akiwa tayari kuwauza Alvaro Morata na Olivier Giroud ili kujihakikishia kutua kwa nyota huyo ambaye kwasasa ana hofu ya kupata nafasi kikosini Juventus mara baada ya klabu hiyo kumnasa Cristiano Ronaldo.
Lakini taarifa nyengine zinadai mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovic ana hofu juu ya usajili huo haswa kutokana na dau ambalo Juventus wanalitaka huku umri wa nyota huyo ukiwa ni miaka 30.
Tajiri huyo anadhani haina haja ya kumsajili mshambuliaji huyo ambaye mwezi Desemba atatimiza miaka 31 huku klabu ikiwa tayari kumuuza Alvaro Morata ambaye kwa umri wake wa miaka 25 bado ana muda mrefu wa kufanya makubwa kuliko kumleta Higuain ambaye atahitaji acheze kwa muda mrefu ili azoee ligi ya Uingereza.
Kocha Maurizio Sarri anamtaka nyota huyo kutokana pia aliwai kuwa naye kwenye klabu ya Napoli kabla ya nyota huyo kusajiliwa na Juventus kwa dau la paundi milioni 75.
No comments:
Post a Comment