Kuna uwepo wa taarifa kwamba Chelsea na klabu nyengine za ligi kuu Uingereza, zimewaambia wachezaji wao ambao wameenda kuzitumia timu zao za taifa barani Amerika Kusini kuwai kurejea kwenye klabu zao.
Inaripotiwa kwamba klabu hizo zimeshindwa kuwazuia wachezaji hao kukataa kuungana na timu zao za taifa kwa kuhofia rungu kutoka shirikisho la soka duniani (FIFA) lakini zimewaomba waweze kujiondoa mapema ili waweze kurejea kutumika kwenye klabu zao.
Ratiba za timu zao za taifa zitaingiliana na ratiba za ligi kuu Uingereza hivyo kuwafanya baadhi ya wachezaji kuchelewa kuzitumikia klabu zao kwenye wiki ya 8 ya ligi kuu Uingereza hivyo kuzifanya klabu zao kutotamani kuwaona wachezaji wao wakitumika mpaka ratiba ya mwisho.
Thiago Silva wa Chelsea na timu ya taifa ya Brazil atacheza mchezo wake wa mwisho na kikosi cha Brazil tarehe 15-Oktoba wakati Chelsea itashuka uwanjani tarehe 16-Oktoba hivyo itakuwa ngumu kwake kuitumikia klabu yake.
No comments:
Post a Comment