Nyota wa Chelsea ambaye ni raia wa Uingereza, Charlie Colckett amekamilisha usajili wake wa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Sherwsburry Town ya nchini Uingereza.
Colckett ambaye ni zao la akademi ya Chelsea hajaweza kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea lakini amekuwa akitumika kutolewa kwa mkopo kwenye klabu kadhaa ikiwemo klabu za Bristol na Vittesse ya nchini Uholanzi.
Nyota huyo mwenye miaka 21 amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mzima akiwaongoza nyota wengine ambao wameshatolewa kwa mkopo. Nyota hao ni pamoja na Eduardo aliyejiunga na Vittesse, Mason Mount aliyejiunga na Derby County, Kenedy aliyejiunga na Newcastle, Reece James, Lewis Baker, Trevoh Chalobah, Dujon Sterling na nyota wengine.
No comments:
Post a Comment