Klabu ya Chelsea inacheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki mchana wa leo huko nchini Australia kwenye jiji la Perth linalopatikana huko magharibi mwa nchi hiyo ikicheza dhidi ya klabu ya Perth Glory.
Mchezo huu unazikutanisha klabu ambazo zote zipo chini ya makocha wapya ambapo kwa Chelsea kuna kocha Maurizio Sarri ambaye leo anatimiza siku 16 toka kuchaguliwa kuwa kocha mpya wa Chelsea akichukua madaraka ya kocha wa zamani ambaye naye ni muitaliano, Antonio Conte wakati kwa klabu ya Perth Glory ambayo ilimtimua kocha wake mara baada ya kuwa na msimu mbovu akimaliza katika nafasi ya nane kwenye ligi yenye timu kumi itakuwa ikiongozwa na kocha Popov ambaye aliwai kuiongoza klabu ya Crystal Palace akiwa kama kocha msaidizi.
Mchezo huu ni maalumu kwa ajili ya kuuzindua rasmi uwanja wa Optus Stadium, uwanja uliojengwa katikati ya jiji hilo la Perth ambao ni uwanja mpya kabisa huku Chelsea dhidi ya Perth Glory ukiwa ni mchezo wa kwanza wa mpira wa miguu kuchezwa kwenye uwanja huu ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000
Mishale ya saa 2:30 mchana (saa 14:30) kwa saa za Afrika Mashariki ndio muda maalumu mchezo huu utashuhudiwa ukichezwa ukiwa ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa Chelsea kabla ya kukutana dhidi ya Inter Milan ambao utakuwa mchezo mwengine wa kirafiki.
No comments:
Post a Comment