Chelsea yaanza vizuri michezo ya kirafiki, yaondoka na ushindi - Darajani 1905

Chelsea yaanza vizuri michezo ya kirafiki, yaondoka na ushindi

Share This

Kikosi cha timu ya Chelsea kimefanikiwa kuondoka na ushindi wake wa kwanza katika mchezo wake wa kwanza wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya ikiibamiza klabu ya Perth Glory bao 1-0.

Mchezo huo ambao ulikuwa mchezo wa kwanza kwa kocha Maurizio Sarri, kiungo mpya Jorginho Frello na mlinda mlango Marcin Bulka umekuwa ulianza saa 2:30 mchana (saa 14:30) kwa saa za Afrika Mashariki uliishuhudia Chelsea ikitumia kwa mara ya kwanza mfumo wa 4-3-3 tofauti na mfumo uliozoeleka wa 3-4-3 uliotumika kwa misimu miwili umeishuhudia Chelsea ikicheza mpira na kuumiliki huku ule mchezo wa kocha Maurizio Sarri wa kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa ukionekana kuanza kuwaingia wachezaji.

Goli hilo la pekee lilifungwa na Pedro Rodriguez mnamo dakika ya tatu ya mchezo akipokea krosi tamu iliyotolewa na kinda Callum Hudson-Odoi na kuifanya Chelsea ipate goli la mapema na la ushindi katika mchezo huo maalumu kwa ajili ya kuufungua uwanja.

Hongereni nyota wetu na sasa ni muda wa kujiandaa ili kucheza mchezo mwengine utakaochezwa tarehe 28-Julai kati ya Chelsea dhidi ya Inter Milan mishale ya saa 9:05 usiku (saa 21:05) kwa saa za Afrika Mashariki. Utakuwa ni mchezo wa kombe la mabingwa wa kimataifa (International Champions Cup-ICC)

No comments:

Post a Comment