Majina ya makipa wengi yameshatajwa mpaka sasa kurithi nafasi ya mlinda mlango nambari moja, Thibaut Courtois klabuni Chelsea.
Petr Cech, Kasper Schmeichel, Pepe Reina, Gigi Donnaruma ni baadhi ya makipa waliotajwa mpaka sasa hivi kurithi nafasi ya mlinda mlango huyo ambaye anatajwa kufukuziwa na klabu ya Real Madrid.
Sasa jina jengine la Jack Butland limetajwa kuingia kwenye orodha ya makipa hao ambao wanafukuziwa na klabu hiyo ya Chelsea.
Butland ni mlinda mlango raia wa Uingereza ambaye ni mlinda mlango wa klabu ya Stoke city na amekuwa akifukuziwa na klabu kadhaa barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment