Willian azidi kufuatiliwa, Chelsea yafunga madirisha - Darajani 1905

Willian azidi kufuatiliwa, Chelsea yafunga madirisha

Share This

Klabu ya Barcelona imekuwa ikimfukuzia nyota raia wa Brazil anayeichezea klabu ya Chelsea, Willian Borges ambaye kwasasa yupo mapumzikoni na familia yake mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia ambapo huko alikuwa akiiongoza timu yake ya taifa.

Klabu hiyo imeshatoa madau kadhaa ili kumsajili nyota huyo ambayo yote yamekataliwa na sasa kuna taarifa imechapishwa na tovuti ya habari za michezo ya Skysports ikidai klabu hiyo imekataa dau la paundi milioni 55 ili kumruhusu mbrazil huyo mwenye miaka 29.

Vyanzo kadhaa vimekuwa vikidai nyota huyo ndiye analazimisha usajili wa kuondoka klabuni Chelsea huku akidhaniwa kutaka kujiunga na Barcelona.

No comments:

Post a Comment