Maurizio Sarri atoa ufafanuzi kuhusu Chelsea kuwabakisha Hazard, Courtois na Willian - Darajani 1905

Maurizio Sarri atoa ufafanuzi kuhusu Chelsea kuwabakisha Hazard, Courtois na Willian

Share This

Klabu za Real Madrid na Barcelona zimekuwa zikitajwa kuwafukuzia nyota watatu wa Chelsea. Eden Hazard na Thibaut Courtois wanafukuziwa na Real Madrid wakati Willian anafukuziwa na Barcelona.

Kutakiwa kwa mastaa hao kumemfanya kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri kulitolea ufafanuzi swala hilo kama je Chelsea itafanikiwa kuwazuia nyota hao wasiondoke?

"Chelsea bado ina mamlaka kuamua nini kitatokea kwa nyota wote wa klabu hii. Nami nahitaji nisalie na nyota wote klabuni ili tufanye vizuri kwenye msimu unaokuja"

"Lakini mimi huwa nina kawaida ya kutaka kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na kila mchezaji, sio mpenzi wa kuongea na mchezaji kwa kupitia simu. Najiamini na naamini nitapata nafasi ya kuongea nao wakisharudi kutoka mapumzikoni" alisema kocha huyo.

Eden Hazard amebakiza mkataba wa miaka miwili ya kusalia klabuni Chelsea huku mwenzake Thibaut Courtois ambaye kwa sasa yupo nchini Hispania akiwa mapumzikoni na familia yake akimaliza mkataba wa kusalia Chelsea mwezi juni mwaka ujao wakati kwa upande wa Willian amekuwa akitajwa kulazimisha usajili wake wa kujiunga na Barcelona.

No comments:

Post a Comment