Kule nchini Urusi kunaendelea michuano ya Kombe la Dunia ambayo imefikia mwishoni ambapo leo kunachezwa mchezo mmoja wa kumtafuta mshindi wa tatu, mchezo utakaochezwa kati ya Ubelgiji dhidi ya Uingereza.
Mchezo huu unazihusisha zile timu zilizopoteza kwenye hatua ya nusu fainali ambapo Ubelgiji ilipoteza dhidi ya Ufaransa kwa goli 1-0 wakati Uingereza ilipoteza mbele ya Croatia ambayo imefanikiwa kutinga fainali kwa mara ya kwanza kwenye michuano hii.
Ubelgiji itakuwa na nyota watatu wa Chelsea ambao ni Eden Hazard, Thibaut Courtois na mshambuliaji aliyetumia nusu msimu uliomalizika akiwa kwa mkopo kwenye klabu ya Borrusia Dortmund, Michy Batshuayi wakati kwa upande wa Uingereza kutakuwa na nyota Gary Cahill ambaye ni nahodha wa Chelsea pamoja na Ruben Loftus-Cheek.
Mchezo huo unachezwa jioni hii saa 5:00 Jioni ( Saa 17:00) kwa saa za Afrika Mashariki.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment