Makala; Hii ndio sababu iliyomfanya Antonio Conte kuondoka Chelsea - Darajani 1905

Makala; Hii ndio sababu iliyomfanya Antonio Conte kuondoka Chelsea

Share This

Huenda hii hukuwai kuifikiria au kuizania. Unadhani nini chanzo cha kocha Antonio Conte kuondoka Chelsea? utanipa majibu mengi nikikuuliza swali hilo, utanambia ni kutokana na kutokuelewana kwake yeye na bodi ya Chelsea, sijakukatalia lakini kuna sababu ya nje kabisa tofauti na hiyo, utanambia kutokana na kuwauza Diego Costa na Nemanja Matic, sina hakika sana katika hilo maana mwenye mamlaka kamili ya maswala ya usajili ni mwanamama Marina Glanovskaia. Au utanambia kutokana na ugomvi unaohisiwa kuwepo kati yake na wachezaji kama David Luiz, sawa haujaenda mbali sana lakini hapohapo nataka nikujuze kitu.

Siamini kama David Luiz ni sababu tosha, kwanini? kwasababu Chelsea haina mipango ya muda mrefu na Luiz kufanya iamue kumuondoa Conte ili imbakize yeye. Na ndio maana ilikuwa tayari kumtumia kama mabadilishano na Koulibaly pamoja na Maurizio Sarri pindi alipokuwa Napoli.

Chelsea imetumia paundi milioni 9 kumlipa Conte kutokana na kuvunja mkataba, imetumia tena paundi milioni 7 kuilipa Napoli kama ada ya Maurizio Sarri, je unazani ingekuwa kuwa tayari kulipa ela zote hizo ili kumridhisha David Luiz mwenye miaka zaidi ya 30? Hapana sio kweli.

Sababu kubwa ukiachana na hiyo ya kutokuwa na mahusiano mazuri na bodi ya Chelsea, sababu iliyomfanya Conte kutimuliwa Chelsea ni kutokana na Eden Hazard na Willian Borges da Silva.

Kivipi?
Unakumbuka mchezo wa ligi kuu msimu uliopita wakati Chelsea ilipokuwa ugenini ikiibamiza Brighton & Hove magoli 1-3? kama unakumbuka vizuri Willian alifunga goli bora la msimu akipigiana pasi vyema na Eden Hazard pamoja na Michy Batshuayi, unakumbuka? baada ya mchezo ule, Hazard na Willian walikabidhiwa kipaza sauti ya chaneli ya Chelsea TV na wote kwa pamoja wanapenda kuchezeshwa pamoja maana wanaendana sana. Huo ulikuwa ujumbe kwa kocha Antonio Conte. Lakini mfumo wa Conte wa 3-5-2 ulikuwa unamfanya Hazard kuanza na Giroud au Morata huku Willian akitokea benchi na mwisho wa siku Willian akaishia kuanza kwenye mchezo 1 kati ya mitano ya mwisho. Tena huo mchezo mmoja alioanza hakucheza mchezo wote akatolewa, ulikuwa wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Southampton na alitoka akiwa amekasirika hakutaka kubaki benchi akapitiliza vyumbani.

Baada ya msimu kumalizika Eden Hazard akaungana na timu yake ya taifa ya Ubelgiji ambapo huko alikutana na rafiki yake Dries Mertens ambaye anaichezea Napoli, tena Napoli hiyo ndio Napoli iliyokuwa inafundishwa na Maurizio Sarri akapewa sifa nyingi kuhusu Maurizio Sarri na jinsi anavyopatana na wachezaji wa Napoli, Hazard aliwai kukiri anatamani kufanya kazi na kocha huyo kutokana na sifa alizopewa na Dries Mertens. Unazani klabu itafanya nini wakati mchezaji wake bora ashasema?

Sio hivyo tu, Willian aliwai kufanya mahojiano na chombo kimoja cha habari na kuulizwa kuhusu kupatana kwake na kocha Antonio Conte, aliishia kucheka na kusema swali hilo atalijibu siku nyengine. Lakini unategemea kipi angekijibu wakati kwenye michezo mitano ya mwisho kaishia kuanza kwenye mchezo mmoja, tena hakucheza mchezo wote aliishia kutolewa.

Na kuna fununu kwamba Willian ndiye analazimisha usajili wake wa kwenda Barcelona, unadhani kwanini Barcelona ilipokataliwa dau la paundi milioni 50 wakaja tena na kutaka kutoa paundi milioni 53? kwa sababu Willian alipata taarifa kwamba Conte karejea klabuni.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment