Hivi ulishawai kufikiri kumiliki klabu katika soka la kisasa? Darajani 1905 tuna ndoto za kumiliki klabu siku moja, klabu itakayokuwa kama tawi la Chelsea nchini Tanzania, kama ilivyo ile klabu ya Ajax ya nchini Afrika Kusini basi nasi tunandoto za siku kumiliki klabu itakayokuwa na mshikamano wa moja kwa moja na klabu ya Chelsea kutoka Uingereza na saajabu tukatikisa sana kwenye soka la bongo.
Acha niache maneno mengi, nirudi kwenye habari. Wakati Darajani 1905 tukiwa na ndoto hizo, huko jijini Tel Aviv nchini Israel kuna tajiri mpya anatikisa kwa sasa. Kuhamia kwake tu kaweka rekodi ya kuwa tajiri zaidi kwenye jiji hilo akiwa anamiliki pia vyanzo vyake kadhaa vya kumuingizia mapesa jijini hapo.
Ushamjua? ni Roman Abramovich, tajiri mwenye uraia wa nchi mbili yaani Urusi na Israel ambako huko ni kutokana na ndugu zake.
Kuna lipi jipya? unaambiwa huyu tajiri wetu anayeimiliki pia klabu ya CSKA Moscow ya huko nchini Urusi ameshafanya kazi na makocha 11 ndani ya miaka 15 toka ainunue Chelsea mwaka 2003.
Sintowataja kwa mtiririko, lakini makocha hao ni Claudio Ranieri ambaye huyo alimkuta, Jose Mourinho, Avram Grant, Felipe Scolari, Andre Villas Boas, Paolo di Matteo, Gus Hiddink, Carlo Ancelotti, Rafa Benitez, Antonio Conte na leo hii ni Maurizzio Sarri.
Yani ndani ya miaka 15 ameshafanya kazi na makocha 11, hii ni sawa na kila kocha kuifundisha Chelsea kwa mwaka mmoja na miezi minne au ni sawa na kusema kila kocha ameifundisha Chelsea kwa miezi 16.
Kocha aliyeifundisha Chelsea kwa muda mrefu ni Jose Mourinho ambaye amedumu miaka 6, ukitoa kwenye ile miaka 15 ambayo Abramovich amedumu na Chelsea unapata miaka 9, kwa maana hiyo hao makocha 10 waliobaki wameifundisha Chelsea kwa miaka 9. Kwenye hao makocha 10 inamaana kila kocha kaifundisha Chelsea kwa miezi 10. Huyu ndiye tajiri wa kirusi bana, hataki mchezo kwenye kazi.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment