Sarri aja na kauli mbiu ya Magufuli. Aanza na mabadiliko - Darajani 1905

Sarri aja na kauli mbiu ya Magufuli. Aanza na mabadiliko

Share This

Tayari ameshakamilisha usajili wake wa kwanza kwa kumsajili mchezaji aliyetoka nae klabu moja, Jorginho sasa aibukia kwenye mabadiliko mengine.

Ndio, taarifa zinaeleza kwamba kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri amepanga kufanya mabadiliko mengine klabuni hapo ikiwa inaelezwa amepanga kumrejesha nyota wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ujerumani, Michael Ballack akitaka kumpa uongozi wa kusimamia maendelea ya soka klabuni hapo (Director of Football).

Nafasi hiyo ambayo mwanzoni ilikuwa ikisimamiwa na Michael Emenalo ambaye kwa sasa yupo klabuni AS Monaco ipo wazi kwasasa huku mwanamama Marina Glanovskaia akiikaimu kwa muda wakati akitafutwa mtu wa kuushika uongozi huo.

Lakini kocha huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuifundisha Chelsea amepanga kumpatia uongozi huo nyota wa zamani wa Chelsea ambaye kwasasa ameshastaafu soka, Michael Ballack huku akisema nafasi hiyo inatakiwa ishikwe na mtu anayeujua mpira na anajua kipi kinatakiwa kwenye soka. Kuja kwa Ballack kutamaanisha Marina Glanovskaia atarudi kwenye majukumu yake ya mwanzo ambapo alikuwa kama mshauri na mtu wa karibu wa tajiri Roman Abramovich.

Kama Michael Ballack akikabidhiwa majukumu hayo, basi atakuwa msimamizi wa usajili kwa wachezaji wanaonunuliwa na kuuzwa na pia atakuwa anasimamia wachezaji wa akademi.

Vipi umeyaonaje mabadiliko haya?

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment