Eden Hazard, Thibaut Courtois na Michy Batshuayi wanafanikiwa kushinda tunzo (medali) zao za kwanza kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea huko nchini Urusi mara baada ya kuitandika Uingereza mabao 2-0 siku ya tarehe 14-Julai katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wakati Ubelgiji ilipomenyana dhidi ya watoto hao wa Malkia.
Eden Hazard aliifungia Ubelgiji goli moja katika mchezo huo huku akiwaacha nyota wenzake wa Chelsea, Ruben Loftus-Cheek na Gary Cahill ambao walikuwa kwenye timu ya Uingereza wakirudi kwao bila medali ya michuano hiyo.
Mchezo huu unamaanisha tupo njiani kwenda kumshuhudia bingwa mpya kwenye mchezo wa soka katika michuano ya Kombe la Dunia ambapo jioni ya tarehe 15-Julai tutashuhudia fainali ya michuano hii itakayozikutanisha timu za Ufaransa dhidi ya Croatia.
Bila shaka mashabiki wengi wa Chelsea tutakuwa upande wa Ufaransa ili kuwashangilia nyota wetu N'Golo Kante na Olivier Giroud watakaokuwa wakiiongoza Ufaransa kwenye mchezo huo.
Lakini pia kama hujawai kujua, kocha wa timu hiyo ya Ufaransa, Didier Deschamps aliwai kuichezea Chelsea toka mwaka 1999 mpaka mwaka 2000 akishinda nayo taji la Kombe la FA.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment