Unaambiwa vipi, Hapa Kazi Tu, eeh kama Magufuli. Hiyo ndio kauli mbiu aliyokuja nayo Maurizio Sarri klabuni Chelsea. Unajua kafanyaje tena?
Kocha huyo ambaye ametambulishwa rasmi kuwa kocha wa Chelsea amemchagua kocha Luca Gotti kuwa msaidizi wake klabuni Chelsea.
Luca Gotti ambaye kwenye maisha yake ya soka ameyatumia akifundisha soka nchini Italia ameteuliwa na Maurizio Sarri kuwa kocha msaidizi wa Chelsea na muda wowote anaweza akaungana na muitaliano mwenzake huyo kuipeleka Chelsea kwenye mstari wa mafanikio.
Luca Gotti mwenye miaka 50 amekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Bologna na sasa anaungana na Maurizio Sarri klabuni Chelsea pamoja na gwiji wa Chelsea, Gianfranco Zola ambaye naye amepewa nafasi ya ukocha kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo.
Umeipenda habari hii?
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment