Hazard, Courtois waanza kuichanganya Chelsea - Darajani 1905

Hazard, Courtois waanza kuichanganya Chelsea

Share This

Leo ndiyo siku ya mwisho kwa michuano ya Kombe la Dunia ambapo kunachezeka fainali kati ya Ufaransa dhidi ya Croatia lakini wakati wa michuano hiyo inapomalizika basi kuna jambo linaenda kutokea pale klabuni Chelsea mpaka kufungwa kwa dirisha la usajili ambalo kwasasa lipo wazi na klabu zinaendelea kusajili.

Ujue ni jambo gani?

Ngoja nikurudishe nyuma kidogo. Mlinda mlango wa Chelsea, Thibaut Courtois pamoja na winga wa Chelsea, Eden Hazard waliwekwa kwenye mazungumzo mara kadhaa ili kusaini mkataba mpya wa kusalia klabuni Chelsea. Lakini mara zote walikataa kusaini.

Ilifikia hatua uongozi wa Chelsea ulikuwa tayari kumlipa Eden Hazard mshahara wa paundi 300,000 kwa wiki na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni ingawa hata sasa bado anaongoza yeye na ilikuwa tayari kumpa Thibaut Courtois mshahara wa paundi 200,000 kwa wiki na kumfanya kuwa kipa anayelipwa zaidi. Lakini bado wote walikataa na walitoa jibu moja kwa pamoja walipokutanishwa, walisema akisaini huyu basi nami nitasaini. Yani Hazard alisema kama Courtois akisaini mkataba mpya wa kubaki Chelsea basi nae atasaini na huyu mwengine nae akasema kama Hazard akisaini mkataba mpya basi nami nasaini.

Basi uongozi wa Chelsea ukaamua kujaribu tena, ikawashawishi wote kwa pamoja, kumbuka huu ni msimu wa mwisho kwa Thibaut Courtois na kwa Hazard mkataba wake unamalizika 2021, na wote wanatajwa kutakiwa na Real Madrid. Lakini baada ya Chelsea kujaribu sana kuwasajili wakaja na jibu jipya wakisema "Subirini kombe la Dunia likimalizika tutakuja na uamuzi mpya" nadhani kufanana kwao kunatokana kwamba wote ni taifa moja la Ubelgiji na ukiangalia klabuni Chelsea wao ndio kama wanamsaada mkubwa kwa klabu.

Haya tumesubiri Kombe la Dunia limalizike na hatimaye wao na timu yao ya Ubelgiji ni kama wamemaliza Kombe la Dunia jana tarehe 14-Julai maana ndio wamecheza mchezo wao wa mwisho na wametwaa ushindi wa tatu.

Unadhani kipi kinaendelea kwa sasa?

Eden Hazard kaulizwa kuhusu kubaki Chelsea anasema anadhani muda wake wa kuondoka ushafika lakini Chelsea ndio watakuwa na uamuzi wa mwisho kama wataamua kumuuza au kumbakisha wakati huku Thibaut Courtois anasema yeye kama yeye anaweza kubaki Chelsea au kuondoka maana kwanza anapapenda London lakini kinachomvuta haswa kuondoka hapo ni kutokana na familia yake kuishi jijini Madrid ambapo huko alipata familia akiwa kwa mkopo Atletico Madrid lakini akamaliza kwa kusema Hazard kasema kama mimi nikiamua kubaki basi nae atabaki.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment