Mishale ya saa 6:00 jioni (saa 18:00) hii leo kutashuhudiwa mchezo utakaoifanya dunia itamani kuona nini kitatokea kwenye mchezo huo wa kumtafuta bingwa mpya wa michuano ya Kombe la Dunia.
Mchezo huo utazihusisha timu mbili kati ya Ufaransa ambao waliwai kuwa mabingwa wa michuano hii mwaka 1998 ambao watashuka uwanjani kucheza dhidi ya timu ya Croatia ambao hii ni mara yao ya kwanza kushiriki fainali ya michuano hii ya Kombe la Dunia.
Lakini kati ya timu hizo kutakuwa na nyota wawili kutoka klabuni Chelsea na wote wamepata fursa ya kuanza katika kikosi cha kwanza katika fainali ya hii leo. N'Golo Kante atakuwa sambamba na nyota mwenzake Olivier Giroud kuisaidia timu yao kushinda michuano hii ambayo inafikia tamati hii leo.
Utabiri wako utakuwa wapi? Ufaransa yenye Kante na Giroud au kwa Croatia?
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment