Kombe la Dunia; Kuelekea fainali, John Terry amtumia Kante ujumbe - Darajani 1905

Kombe la Dunia; Kuelekea fainali, John Terry amtumia Kante ujumbe

Share This

Kila mtu sasa anazungumzia mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia, basi nasi Darajani 1905 hatuna budi kunyamaza kukuletea habari nyengine zaidi ya mchezo huu kati ya Ufaransa dhidi ya Croatia mpaka pale utakapomalizika.

Kuelekea kwenye mchezo huo ambao umebakiza muda kidogo kabla ya kuanza, nyota wa zamani wa Chelsea, John Terry ametumia akaunti yake ya mtandao wa Instagram kumtakia heri nyota wa Chelsea, N'Golo Kante ambaye atakuwepo kwenye mchezo huo kwa upande wa timu ya Ufaransa.

Terry ametuma picha ya kiungo huyo mkabaji akiwa na kombe la ligi kuu msimu wa 2016-2017 akiwa klabuni Chelsea huku akiandika maneno yanayosomeka ya kumsifia huku akidiriki kusema kama angekuwa yeye ndiye kocha basi angeitengeneza timu juu ya kiungo huyo.

Utaniuliza kwanini hajatuma picha ya nyota huyo akiwa na timu yake ya Ufaransa? ntakujibu kwa ufupi tu kwa vile yeye ni mchezaji wa zamani wa Uingereza na timu yake imetolewa😁😁😁 nimekujibu vizuri? aah natania tu

Au utaniuliza kwanini hajatuma na picha ya Olivier Giroud ambaye naye ni mchezaji wa Chelsea? nitakujibu kwa vile wakati Terry anacheza Chelsea, Giroud alikuwa bado hajasajiliwa, bila shaka nipo sawa, au sio? Tukutane baada ya mchezo kuisha..

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment