Kombe la Dunia; Kante, Giroud waibuka mashujaa, Ufaransa ikiibuka mabingwa - Darajani 1905

Kombe la Dunia; Kante, Giroud waibuka mashujaa, Ufaransa ikiibuka mabingwa

Share This

Timu ya taifa ya Ufaransa inafanikiwa kutwaa ubingwa wake wa pili wa Kombe la Dunia mara baada ya kuibamiza timu ya Croatia magoli 4-2 jioni hii ya leo.

Ushindi huu unamaanisha nyota wa Chelsea, N'Golo Kante na Olivier Giroud wanafanikiwa kuibuka mabingwa kati ya nyota wa Chelsea walioshiriki michuano hiyo kwa mwaka huu ambapo klabu hiyo ilitoa wachezaji 14 kushiriki katika michuano hiyo kwa timu mbalimbali.

Eden Hazard, Thibaut Courtois na Michy Batshuayi waliiongoza Ubelgiji, Victor Moses na Kenneth Omeruo waliiongoza Nigeria, Ruben Loftus-Cheek na Gary Cahill waliiongoza Uingereza, Willian Borges aliiongoza Brazil, Antonio Rudiger akiiongoza Ujerumani, Willy Caballero aliiongoza Argentina, Cesar Azpilicueta akiwa Hispania, Andreas Christensen aliiongoza Demmark huku Kante na Giroud wakiiongoza Ufaransa.

Hongereni kwa nyota wote wa Chelsea sasa kinachofuata ni kujiandaa na michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya wa 2018-2019.. Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment