Kombe la Dunia; Eden Hazard, Thibaut Courtois waibuka vinara, washinda tunzo - Darajani 1905

Kombe la Dunia; Eden Hazard, Thibaut Courtois waibuka vinara, washinda tunzo

Share This

Michuano ya Kombe la Dunia imemalizika kwa Ufaransa kuibuka mabingwa mara baada ya kuondoka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Croatia kwenye mchezo wa fainali uliochezwa jioni ya leo.

Wakati Olivier Giroud na N'Golo Kante wakiiongoza Ufaransa kushinda michuano hiyo lakini nyota wengine wa Chelsea, Thibaut Courtois na Eden Hazard ambao ni nyota wa timu ya Ubelgiji walioshinda nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo wameibuka vinara katika tunzo za michuano hiyo.

Thibaut Courtois ambaye ni mlinda mlango amefanikiwa kushinda tunzo ya mlinda mlango nambari moja wa michuano hiyo akiwa ni kipa bora wakati Eden Hazard akishinda tunzo ya mchezaji bora kwa nafasi ya pili (silver ball) wakati mchezaji bora wa mashindano akiibuka Luca Modric wa Croatia.

Lakini tunzo hii haijaenda kwa Hazard ambaye mwanzoni alikuwa akitajwa kukaribia kuishinda kutokana na washindani wake kufanikiwa kufika fainali. Luca Modric amefanikiwa kucheza fainali akiwa na Croatia wakati Antoinne Griezman aliyechukua nafasi ya tatu akiiwezesha Ufaransa kufika fainali na kuwa mabingwa.

Vipi una maoni gani katika hili?

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment