Chelsea yatenga dau nono kumnasa nyota wa Juventus - Darajani 1905

Chelsea yatenga dau nono kumnasa nyota wa Juventus

Share This

Klabu ya Chelsea imeingia sokoni ili kuanza kuijenga timu mara baada ya kumpata kocha mpya Maurizio Sarri ambaye alitambulishwa rasmi siku ya jumamosi tarehe 14-Julai.

Klabu hiyo inatajwa kuingia sokoni na kumfukuzia mshambuliaji raia wa Argentina anayeichezea klabu ya Juventus ya nchini Italia, Gonzalo Higuain.

Higuain ambaye aliwai kuwa nyota wa klabu aliyotokea kocha wa sasa wa Chelsea, klabu ya Napoli kabla hajajiunga na Juventus anatajwa kutengewa dau la euro milioni 60 ili atue Chelsea kabla ya kuanza kwa msimu mpya ambao Chelsea itakuwa inashiriki michuano minne ambayo ni Ligi ya Ulaya (Europa League), ligi kuu Uingereza, Kombe la FA na kombe la ligi.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment