Klabu ya Chelsea inatajwa na gazeti la The Times kuwa klabu itakayoweka rekodi mpya nchini Uingereza ambapo inaitaja klabu hiyo kuingia kwenye mpango mpya wa kibiashara katika swala la udhamini.
Klabu hiyo inatajwa kuingia kwenye makubaliano na kampuni ya magari ya Hyundai ambapo kampuni hiyo inatajwa kuingia mkataba wa miaka mitano na klabu ya Chelsea wenye thamani ya paundi milioni 50 ambao utaifanya Chelsea kuvuta dau nono zaidi kutoka kwa mdhamini kuliko klabu yoyote nchini Uingereza huku ikiwa ni mara mbili ya dau wanalolipokea Manchester city kutoka kwa Nixen.
Lakini udhamini huu ni tofauti na ule udhamini ulionao Chelsea na kampuni ya matairi ya Yokohama ambao ndio wadhamini wakuu wa Chelsea kwa sasa huku wakibakiza miaka miwili kwenye mkataba wao wa sasa wenye thamani ya paundi milioni 200.
Tofauti ipo wapi? Chelsea imeingia mkataba na kampuni ya magari ya Hyundai ambao wenyewe watakua wanatangaza katika upande wa jezi au fulana za Chelsea kwa upande wa kushoto wa fulana hizo ambapo mwanzoni kulikua na tangazo la Alliance Tyres ambapo Chelsea ilitoa ofa kwa kampuni ya Yokohama kuitangazia sehemu ya matairi hayo yanayojulikana kama Alliance. Kwa maana hiyo kampuni ya Yokohama Tyres ilipewa ofa ya kutangaza matairi yake ya Alliance Tyres kwa msimu mmoja tu wa 2017-2018 na mara baada ya msimu huo kuisha ndipo udhamini wa Hyundai kwa klabu ya Chelsea utakapochukua nafasi kutangaza katika ule upande uliokuwepo tangazo la matairi ya Alliance.
Dili hili bado halijatangazwa rasmi na klabu ya Chelsea lakini gazeti hilo la The Times ndilo limeripoti taarifa hizo ambapo kama mpango ukikamilika basi Chelsea itakua klabu inayovuta pesa ndefu kupitia udhamini wa mikono ya fulana ya jezi zao ambazo kwa sasa zinatengenezwa na kampuni ya Nike.
Kwa dili hili likikamilika litamaanisha Chelsea sasa itakuwa na wadhamini wa matairi ya magari (Yokohama Tyres), kampuni ya kuuza magari (Hyundai) na kampuni ya vinywaji vya kuongeza nguvu 'energy drinks' (Carabao) ambao hawa wao wanatangaza haswa kupitia jezi za mazoezi.
No comments:
Post a Comment