Kwaheri gwiji wetu, asante kwa kuiongoza vyema Chelsea - Darajani 1905

Kwaheri gwiji wetu, asante kwa kuiongoza vyema Chelsea

Share This

Nyota na nahodha wa klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea Ladies, mwanamama Katie Chapman ametangaza kustaafu kucheza soka ifikapo mwishoni mwa msimu huu mara baada ya kuiongoza Chelsea kwa miaka mitatu akiwa kama nahodha wa kikosi hicho.

Mwanamama huyo ambaye ni mzazi wa watoto wa kiume watatu aliozaa nao pamoja na mme wake Mark ametangaza kustaafu kucheza soka ifikapo mwishoni mwa msimu huu huku akitengeneza historia na heshima kubwa nchini Uingereza huku akifananishwa na gwiji wa kikosi na nchini humo, David Beckham.

Chelsea ilimsajili nyota huyo mwenye uwezo wa kucheza kama kiungo wa kati na hata akitumika kama mlinzi wa kati anastaafu kucheza soka huku akiwa na rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyewai kutwaa taji la kombe la FA kwa wanawake kwa mara 10 ambapo alitimiza mara hiyo ya kumi siku kadhaa wakati alipoiongoza Chelsea kuibamiza klabu yake ya zamani ya Arsenal Ladies katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley kwa magoli 3-1 ambapo magoli ya Chelsea yalifungwa na Fran Kirby pamoja na mshambuliaji mwenzake Ramona Bachmann aliyefunga mara mbili.

Jambo ambalo huenda hulijui kuhusu nyota huyu mwenye miaka 35 kwa sasa, aliwai kucheza timu moja na pacha wake kwenye klabu ya Millwall Lioness ambako huko ndipo alianzia maisha yake ya soka la ushindani.

Hongera gwiji wetu...

No comments:

Post a Comment