Kocha Antonio Conte bado anatajwa na magazeti mengi barani Ulaya kuwa hatoendelea kusalia klabuni Chelsea kama kocha wa klabu hiyo kwa msimu ujao.
Kocha huyo anatajwa kutokua na mawasiliano mazuri na bodi ya klabu hiyo akiishutumu juu ya mpango wake wa usajili inaoufanya kwa klabu hiyo. Majukumu ya usajili klabuni Chelsea yanaonekana yapo chini ya bodi ya klabu hiyo ambapo majukumu yote yamewekwa chini ya mwanamama Marina Glanovskaia ambae yeye ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya usajili wa klabuni hapo.
Kuondoka kwa kocha huyo klabuni Chelsea halionekani kuwa ni jambo zuri kwa kiungo na nyota wa klabu hiyo ambaye alisajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili lililopita ambapo aliigharimu Chelsea kiasi cha paundi milioni 40 akitokea As Monaco ya nchini Ufaransa ambapo huko ndipo utaifa wake ulipo, Tiemoue Bakayoko.
Nyota huyo amefanyiwa mahojiano akiulizwa juu ya nini anakiwaza kama kocha huyo ataachana na klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu.
"Kiukweli sifatilii sana juu ya taarifa hizo. (Conte) hakuwai kusema jambo ilo, mara zote amekua akitazamia kushinda na kufanya vizuri kwenye msimu mzima"
"Kama mchezaji, nimekua sipendezwi (kama akiondoka). Wote tunapenda kufanya kazi na kocha kama huyu na kuwa na mahusiano na kocha kama huyu kwa muda mrefu. Nimefanya nae kazi kwa mwaka mzima na nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa nikiwa chini yake ila maamuzi yapo chini ya uongozi wa klabu, yeye mwenyewe lakini kwa kusema kama anataka kuondoka, hilo hajawai kulizungumza" alisema kiungo huyo.
No comments:
Post a Comment