Moja kati ya picha bora sana kutoka kwenye mechi ya jana!
Utamu wa hii picha upo hivi!
Huyo unayemuona akiwa na jezi za Southampton, ni mchezaji kinda aliyekuzwa na kulelewa na akademi ya Chelsea, anaitwa Tino Livramento, msimu uliopita ndiye alikuwa mchezaji bora kwenye akademi ya Chelsea, akicheza nafasi ya beki wa kulia.
Tino amejiunga na Southampton kwenye dirisha hili lililopita la usajili, na toka amejiunga na klabu hiyo amekuwa na msimu mzuri akifanya makubwa na ata jana alikuwa bora sana.
Kwa mtazamo wangu, kabla hatujafunga goli la pili, nilimtazama yeye kama angechaguliwa kuwa nyota wa mchezo kutokana na makubwa aliyoyafanya!
Unakumbuka kuna lile shambulizi la Hudson-Odoi alilobaki yeye na kipa? huyu dogo alitokea nyuma kabisa akaja kuzuia shambulizi kali kishenzi.
Alifanya 'block' za maana kama mbili hivi kama nitakuwa sikosei, na bado akasababisha penati ya Southampton waliyopatia goli.
Sasa jana ulikuwa mchezo wake wa kwanza kucheza ndani ya Darajani uku akiwa timu pinzani, na aliuwasha moto hatariiii!
Kwenye mkataba wake kuna kipengele cha kusajiliwa tena na Chelsea endapo wakimtaka huko baadae, na dau lililopo kwenye mkataba ni euro milioni 50 lakini litapungua na kufikia euro milioni 35 sababu fungu jengine itatakiwa ilipate Chelsea kutokana na Chelsea kutakiwa kufaidika endapo nyota huyo atauzwa kwenda poppte.
Liweke jina lake kwenye kumbukumbu zako maana wachezaji wote walioshinda tuzo ya mchezaji bora wa akademi wamekuwa wakiuwasha moto sana, Mason Mount, Billy Gilmour, Conor Gallagher, Reece James na ata Fikayo Tomori kule AC Milan huwaambii kitu aliyepotea ni Dominic Solanke tu!
No comments:
Post a Comment