"ni vizuri kwa mchezaji kuhusika katika mchezo mkubwa kama huo, nami nwajua Bacelona maana nilipokuwa kwa mkopo Borrusia Monchlegbach tulimenyana nao ambapo katika mchezo wa kwanza tuliwatangulia 1-0 kabla ya baadae kutufunga magoli 2 na mchezo kuisha kwa kupoteza 2-1, utakuwa mchezo mzuri na mgumu kwa timu zote" alisema Christensen ambaye ametokea kwenye akademi ya Chelsea kabla ya kupelekwa kwa mkopo kwenda Borrusia Monchlegbach ambapo huko alicheza kwa misimu miwili.
"huwa siangalii historia na takwimu zinasemaje, ninaingia kwenye mchezo nikiwa na kitu kimoja tu kichwani, natakiwa kuifanya timu yangu ipate kile inachokitaka" alimalizia Christensen.
Chelsea itamenyana na Barcelona mwezi februari mwakani huku historia ikiziweka sawa klabu hizo ambapo jumla zimekutana mara 15 huku Chelsea akishinda michezo 5 na kutoa suluhu 5 huku Barcelona nae akishinda michezo 5.
No comments:
Post a Comment