CHELSEA KUUFUNGUA UWANJA MPYA - Darajani 1905

CHELSEA KUUFUNGUA UWANJA MPYA

Share This
Huenda umepata taarifa kupangwa kuchezeka mchezo wa kirafiki kati ya Chelsea dhidi ya klabu ya nchini Australia ya Perth Glory, ambao mchezo huo ni wa kirafiki na umepangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Optus Stadium ambao una uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 mpaka 65,000 umefunguliwa tarehe 28-Januari mwaka huu, na Chelsea ndio itakuwa timu ya kwanza ya soka kucheza kwenye uwanja huo mpya kabisa.

Nyota wa zamani wa Chelsea, Mark Schwazer ambaye ni raia wa nchini humo amefurahi kupata taarifa hizo na alipohojiwa alisema amefanya mawasiliano na wachezaji wa Chelsea juu ya maoni yao kuhusu kupnagwa kucheza mchezo huo mpya kabisa na anasema kila mchezaji wa Chelsea amefurahishwa juu ya taarifa hizo.

Mchezo huo utachezwa tarehe 23-Julai mwaka huu.


No comments:

Post a Comment