Nyota wa Chelsea, Marcos Alonso Mendoza jana aliichezea kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya Hispania kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Argentina na kuiongoza vyema timu yake kupata ushindi wa magoli 6-1. Mara baada ya nyota huyo kufanikiwa kucheza mchezo huo akiingia kama mchezaji wa akiba akichukua nafasi ya Jordi Alba.
Nyota huyo amefanikiwa kuweka historia na kuwa na mafanikio makubwa tangu atue klabuni Chelsea mwaka 2016 lakini pia akifanikiwa kuweka historia mpya katika maisha yake ya soka lakini pia kwa familia ambapo anaendeleza kizazi bora kutokana na baba yake na babu yake kuwai pia kuichezea timu hiyo ya taifa.
Kupitia mtandao wa Instagram, nyota huyo anayecheza nafasi ya ulinzi wa kushoto alituma ujumbe kuonyesha furaha yake ya ushindi ilioupata timu yake ya Hispania, lakini pia kuonyesha furaha kwa kuichezea kwa mara ya kwanza timu hiyo na kuweka historia kubwa.
Nasi kama mashabiki wa Chelsea tunajitoa kwa kusema hongera kwake👏👏👏
No comments:
Post a Comment