Jana ilikuwa siku ya michezo ya kirafiki kwa timu za kimataifa na kama ilivyoada wachezaji wa Chelea nao waliungana na timu zao za taifa ili kucheza michezo ya timu zao za taifa na hapa nakuletea baadhi ya matukio yanayowahusu wachezaji wa Chelsea wakiwa kwenye timu zao hizo.
Michy Batshuayi aliiongoza vyema timu yake ya taifa ya Ubelgiji kupata ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya timu ya Saudi Arabia, Willian Borges aliyeiongoza Brazil naye akausika kutoa pasi iliyozaa goli pekee katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani lakini pia Marcos Alonso akafanikiwa kuichezea Hispania mchezo wake wa kwanza akiingia kama mchezaji wa akiba akichukua nafasi ya Jordi Alba na kufanikiwa kuihakikishia timu yake hiyo kupata ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Argentina lakini pia Cesar Azpilicueta nae akiingia kama mchezaji wa akiba kwa timu ya Hispania.
N'golo Kante na Olivier Giroud nao wakaiongoza vyema timu yao ya Ufaransa kupata ushindi wa mabao 2-3 wakati Davide Zappacosta nae akiingoza vyema timu ya Italia kupata suluhu ya 1-1 dhidi ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment