HERI YA KUZALIWA ALUKO - Darajani 1905

HERI YA KUZALIWA ALUKO

Share This
Miaka 31 iliyopita, katika jiji la Lagos pale nchini Nigeria, alizaliwa mtoto wa kike ambaye leo ni nyota mkubwa kwenye klabu kubwa barani Ulaya, Eniola Aluko, mwanadada anayeichezea Chelsea ya akina dada maarufu kama Chelsea Ladies ambayo inashiriki ligi kuu kwa akina dada pale Uingereza.

Nyota huyo alianza kucheza soka Leafield Athletic ambapo hapo alicheza soka lake la ujanani kabla ya kujiunga na klabu ya Birmingham Ladies, ambapo aliichezea klabu hiyo kutokana na kukulia kwenye jiji hilo la Birmingham kwa muda mrefu toka alipotoka nchini Nigeria toka akiwa na mwaka mmoja.

Alicheza hapo mpaka alipojiunga rasmi na Chelsea Ladies mwaka 2007, kipindi iko alikuwa na miaka 20, ambapo alicheza hapo mpaka mwaka 2009 kabla ya kuja kurudi tena mwaka 2012, na toka kipindi iko mpaka sasa bado yupo Chelsea Ladies na amefanikiwa kuahinda mataji kadhaa kwa upande wa klabu na yeye mwenyewe binafsi.

Jambo usilolijua kuhusu nyota huyu, baba yake aliwai kuwa mbunge wa bunge la nchini Nigeria lakini pia nyota huyu anashikilia shahada ya kiwango cha juu (First Class Degree) ya mambo ya Sheria ambayo aliisomea kwenye chuo kikuu cha Brunel kilichopo nchini Uingereza magharibi mwa jiji la London. Sasa uwe makini, huenda ukakutana nae pale kwenye mahakama ya Kisutu ukashangaa.

Heri ya kuzaliwa kwako Aluko.

No comments:

Post a Comment