ANCELLOTTI ATUA CHELSEA - Darajani 1905

ANCELLOTTI ATUA CHELSEA

Share This
Wakati jana Chelsea iliposhuka uwanjani kumenyana dhidi ya Barcelona, ambapo mchezo huo uliisha kwa sare ya 1-1 katika nngwe ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya. Mchezo huo ulitazamwa na wengi na wengi wakitamani kuona je itakuwaje katika mchezo huo uliotajwa kuwa mchezo uliosubiriwa na wengi.

Katika mchezo huo uliotazamwa na wengi, lakini pia kulikuwa na watazamaji wawili marafiki waliowai kufanya kazi pamoja klabuni Chelsea. Ni Carlo Ancellotti, ambaye aliwai kuwa kocha wa Chelsea huku msaidizi wake akiwa Paul Clement a,mbaye naye alikuwa pembeni ya kocha huyo raia wa Italia.

Kupitia mtandao wa Twitter, kocha huyo alituma ujumbe akiwa kwenye uwanja wa stamford Bridge kama mmoja wa watazamaji huku pembeni akiwepo kocha Paul Clement ambaye alikuwa msaidizi wake pindi walipokuwa klabuni Chelsea na kufanikiwa kutwaa taji la ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2009-2010.

Alituma ujumbe uliosomeka, "Nikiwa kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa usiku huu, nimefurahi kuwa pamoja na rafiki yangu Paul Clement. #UCL"

No comments:

Post a Comment