CHELSEA LADIES KUELEKEA MCHEZO WA LEO vs YEOVIL - Darajani 1905

CHELSEA LADIES KUELEKEA MCHEZO WA LEO vs YEOVIL

Share This
Mara baada ya kutoka kupata ushindi wake mnene dhidi ya Doncaster katika mchezo uliopita kwa mabao 6-0, klabu ya akina dada ya Chelsea ladies itashuka tena leo uwanjani kupambana katika mchezo wa ligi kuu ya wanawake ya nchini Uingereza ambapo watapambana dhidi ya klabu ya Yeovil ambapo mchezo huo utachezwa saa 09:45 usiku (Saa 21:45).

Chelsea Ladies itashuka uwanjani kupambana na klabu hiyo katika mchezo huo wa ligi kuu kwa upande wa wanawake, na inahitaji ipate ushindi ili ijiweke sawa katika msimamo wa ligi hiyo ambapo kwa sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo na kama ikipata ushindi katika mchezo huo ambao inacheza dhidi ya Yeovil wanaoshika mkia katika msimamo huo, basi itafanikiwa kushika usukani wa ligi hiyo ambayo kwa sasa nafasi hiyo inashikwa na Manchester city Ladies ambao wao wana alama 25 wakati Chelsea Ladies wana alama 23.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kiungo mkabaji wa Chelsea Ladies, Maren Mjelde ametoa neno kuhusu mchezo huo, "Ji kiasili ni kiungo ambaye yupo vizuri sana kwenye kushambulia, kwa hiyo kama nnacheza pamoja nae huwa najihisi nina majukumu ya kukaba zaidi na kuimarisha zaidi kwenye safu ya ulinzi kuliko kushambulia" alisema alipohojiwa juu ya mahusiano yake uwanjani na nyota wa klabu hiyo, Ji So-Yun ambaye amekuwa na kiwango bora huku akitoka kufunga magoli matatu katika mchezo uliopita ambao walishinda 6-0 dhidi ya Doncaster ambapo Mjelde alitumika kama mchezaji wa akiba na kuingia katikati ya mchezo.

"Lakini napocheza pamoja na Katie (Chapman), anaweza akapanda mbele kusaidia mshambulizi nami nikabaki nyuma kusaidia ukabaji, au nami naweza kwenda mbele kusaidia mashambulizi naye akabaki kama mkabaji. Sisi kwa pamoja kiasili ni wakabaji."

"Naamini tuna viongozi wengi kwenye timu yetu wanaopaswa kuwa manahodha lakini kama nahodha mkuu asipocheza au kuwepo kwenye mchezo basi ndio wakati timu inapotakiwa kucheza kwa majukumu ya ziada . Na nililiona hilo katika mchezo dhidi ya Doncaster"

"Nimekuwa kwenye mapumziko nikipata nafasi mara ya mwisho toka mchezo dhidi ya Man city, na najiona sasa nipo sawa na naweza kurejea kwenye nafasi yangu. Nahitaji kurudi tena uwanjani na kuendelea kupambana. Mchezo wetu wa pili dhidi ya Man city unakaribia na nataka kujiandaa na kucheza ili niwe sawa kuchez a dhidi yao" alisema Mjelde

Kiungo huyo amekuwa akitumika kwenye kikosi hicho cha akina dada kabla ya kupata majeraha yaliyomweka nje na kumfanya kutumiaka kama mchezaji wa akiba, lakini sasa amerejea na anataka kucheza ili kupambania taji hilo la ligi kuu Uingereza kwa upande wa wanawake.

Na kwa hatua ya robo fainali ya kombe la FA, klabu ya Chelsea Ladies ilipangiwa kupambana na Liverpool Ladies katika hatua hiyo ya robo fainali mara baada ya kupata ushindi mnono dhidi ya Doncaster.

No comments:

Post a Comment