BAILEY ATOA NENO KUTAKIWA NA CHELSEA - Darajani 1905

BAILEY ATOA NENO KUTAKIWA NA CHELSEA

Share This
Winga mjamaika, Leon Bailey ambaye anaichezea klabu ianyoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga, klabu ya bayer Leverkusen ametoa neno mara baada ya kuhusishwa kwa kipinid kirefu kuwa chaguo na penekezo la kocha Antonio Conte ili atue Chelsea, akitazamiwa kutua katika dirisha kubwa la usajili.

Nyota huyo alipohojiwa juu ya kutakiwa kwake na Chelsea alisema "Kwa sasa najihisi kuwa sawa nikiendelea kubaki Leverkusen. Nataka niendelee kukua na kukomaa nikiwa hapa, kisha baadae nichukue hatua nyengine."

"Kama nikijiunga na klabu kubwa kwa sasa, watu watataka kujua mimi ni nani, sitaki iwe ivyo, nataka nikijiunga kwenye klabu basi watu wawe tayari wanajua mimi ni nani" alisema winga huyo.

Bailey alikuwa akicheza klabu moja na mtanzania, Mbwana Samatta katika klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji kabla ya nyota huyo kuamia Ujerumani na kumwacha Samatta akiendelea kupambana klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment