PULISIC, BATSHUAYI BADO HAKIJAELEWEKA - Darajani 1905

PULISIC, BATSHUAYI BADO HAKIJAELEWEKA

Share This
Klabu ya Borrusia Dortmund imevutiwa na mshambuliaji wa Chelsea, Michy Batshuayi anayecheza klabuni hapo kwa mkopo ambao utaisha mwisho wa msimu akiichezea klabu hiyo michezo minne huku akiifungia magoli matano, anatazamwa kama mrithi sahihi kwa klabu hiyo akiziba pengo la mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo alieungana na Arsenyani (Arsenal), Pierre Aubameyang.

Kutokana na kuvutiwa na nyota huyo, klabu hiyo ikapeleka maombi kwa Chelsea ili imsajili kabisa mshambuliaji huyo mwenye miaka 24 kwa sasa ili ajiunge kabisa na klabu hiyo, lakini taarifa zikatoka kuwa Chelsea imegoma kumuuza. Lakini baadae tena ikatoka taarifa kuwa Chelsea imekubali kumuachia mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji ajiunge na klabu hiyo lakini kwa mabadilishano na mchezaji wa klabu hiyo ambaye ni raia wa Marekani, Christian Pulisic.

Taarifa hizo zikazagaa kwa karibu zikieleza Chelsea inamtaka winga huyo ili ajiunge na klabu hiyo ya London kwa kubadilishana na Batshuayi, taarifa nyengine zimetoka kuwa klabu ya Ujerumani, Bayern Munich na wao wanamuwania nyota huyo ili ajiunge na klabu hiyo. Sasa kinachosubiriwa ni hatua za mwisho, kipi watakiamua Dortmund kama kumuuza nyota huyo aende kwa watani wao au laah wakubali ajiunge na Chelsea ili wao wabaki na Batshuayi.

No comments:

Post a Comment