MSIKIE ALICHOKISEMA COURTOIS KUTAKIWA KWAKE NA MADRID - Darajani 1905

MSIKIE ALICHOKISEMA COURTOIS KUTAKIWA KWAKE NA MADRID

Share This
Mlinda mlango wa Chelsea, Thibaut Courtois aliiongoza vyema klabu ya Chelsea kupata suluhu katika mchezo wa jana dhidi ya barcelona ambao ulikuwa ni mchezo wa raundi ya 16 bora katika klabu bingwa barani Ulaya, mchezo ulioisha kwa suluhu ya 1-1.

Mara baada ya mchezo huo, mlinda mlango huyo alifanyiwa mahojiano na kuulizwa kuhusu kauli yake ya kusema moyo wake upo Madrid huku kukiwa na tetesi za kutakiwa na klabu ya Real Madrid inayotajwa kumfukuzia kwa muda mrefu.

Nyota hyo alipohojiwa juu ya kauli hiyo, alisema "Nilieleweka tofauti juu ya kauli hiyo. Familia yangu inaishi Madrid, nami nipo huku, sio jambo rahisi kwangu. Bado nina mwaka mmoja kwenye mkataba wangu (kwa Chelsea) na nina furaha kubaki hapa"

"Na kama kuna taarifa juu ya kutakiwa kwangu na Real Madrid basi nadhani Fiorentino Perez (rais wa klabu ya Real Madrid) basi hatonipigia mimi, ataongea na wakala wangu ili kufanya nae amzungumzo" alisema nyota huyo mwenye miaka 25 kwa sasa.

Nyota huyo aliwai kuishi kwenye jiji la Madrid nchini Hispania alipokuwa uko kwa mkopo akitokea Chelsea, ambapo alikuwa akiichezea klabu ya Atletico Madrid na kufanikiwa kujenga familia ambayo bado ipo nchini humo.

No comments:

Post a Comment