Chelsea inamfukuzia kiungo raia wa Ivory Coast anayekipiga pale kwenye klabu ya OGC Nice ya nchini Ufaransa, Jean Michael Seri lakini inaonekana kupata upinzani mkubwa kutoka kwa klabu ya Arsenal ambayo nayo inatajwa kumtamani nyota huyo.
Lakini jambo linaloonekana kuiharibia Chelsea katika kutaka kwake kuinasa saini ya kiungo huyo ni kushindwa kuwa na uhakika katika nafasi yake ya ukocha ambapo mpaka sasa bado haijaeleweka kama itaendelea kusalia na kocha wake Antonio Conte au itamchukua kocha mwengine kurithi nafasi ya kocha huyo kikosini hapo.
Wakati kwa upande wa Arsenal inaonekana kupewa nafasi kubwa haswa kutokana na moja ya viongozi klabuni hapo aliyejiunga akitokea Barcelona kuwa na mahusiano mazuri na kiungo huyo haswa mahusiano yanayochochewa na kujaribu kwake kumnasa kipindi kile alipokuwa klabuni Barcelona ambapo ilibaki kidogo kiungo huyo ajiunge na klabu hiyo ya Barcelona.
Lakini kwa upande wa wakala wake aliwai kukaririwa akisema anamwamini mchezaji huyo na mara zote amekuwa akijiunga kwenye klabu anayoona inafaa.
No comments:
Post a Comment