Wengine tupo bongo bahati mbaya, ndio maana kuna wengine wanasemaga kuliko kuwa mtanzania ni bora awe mbwa uko Marekani...mtoto wa maskini kama mimi nimeamua kujiajiri kupitia blog tena kwa ubunifu wangu mkubwa unanambia nitoe mamilioni ili nipate kibali wakati nimekosa laki 8 ya kwenda kusomea IT inakuwa ni kama unaukamua mfuko wa rambo ili utoe maziwa...blog yenyewe haijanilipa hata senti 5 zaidi ya mimi kufanya kazi za juani ili kutafuta ela ya vocha ili niweke nipost kile nachoamini baada ya miaka mitano kitaniweka sehemu nzuri mimi na familia yangu!!! unataka nikakabe ili kesho useme vijana hatufai??? unataka nikauze unga ili uje unikamate useme kwanini nauza unga???
Kama uchochezi au maudhui yasiyofaa basi ungefanya usajili kama ulivyofanywa usajili wa laini na sio kutufungia kwa kutuambia tutoe pesa ambazo hata familia yangu haijui itazishika lini..unataka baadae nikifanikiwa nirudi kuwekeza Tanzania??? blog yangu ni ya michezo tena ya Ulaya, nimeangaika kupata ranking ya Google, Mungu kanisaidia nimeanza kuonekana bado unakuja unanambia nitoe mamilioni, kweliii??? mbona daraja la wenyenacho na wasiokuwa nacho linazidi kuongezeka badala ya kupungua??? kwa style hii huyo mwenye nacho atalipia atapata kibali vipi miye nisiyekuwa nacho na nimekuwa nikiangaika mpaka kuamka saa 9 usiku ili kusaka habari mpya nizitume????
Nimeamua kufanya blogging kwa kuwa ni kipaji changu lakini pia kwa kuwa ninapenda IT na hii ndio nafasi yangu pekee kufanya kazi inayoendana na kile nachokipenda lakini kama nitahukumiwa kwa kile nachokipenda, kama nitawekwa ndani kwa kile nachokipenda basi acha lolote litokee kwangu lakini blogging siwezi kuacha maana nitakuwa naachana na kile nachokipenda. Nitakuwa sawa naachana na mwanamke mzuri ambaye duniani sijaona wakufanana nae. Chozi la mnyonge.
#VivaTanzania
No comments:
Post a Comment