Mara baada ya Chelsea kumfukuzia winga wa klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa, Thomas Lemar, sasa klabu hiyo imetoa majibu kamili kuhusu nyota wake huyo kuelekea katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo la usajili la mwezi januari.
Akizungumza mara bada ya kuhojiwa kuhusu mipango ya nyota huyo, makamu wa rais wa klabu ya AS Monaco ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Ufaransa maarufu kma Lige 1, ndugu Vadim Vasilyev amesema "hatuna mipango hiyo kwa sasa, hatuna mipango ya kuuza nyota yoyote kwa sasa. Tumeshaanza kuwa na mfumo mzuri, tunawaza kuhusu mafanikio ya timu na sio kuuza nyota wetu katika dirisha hili la januari"
AS Monaco imekuwa na mfululizo wa matkeo mbovu msimuu huu mara baada ya kuwauza nyota wake kama Tiemoue bakayoko aliyekuja Chelsea, Bernardo Silva aliyeenda Manchester city pamoja na Benjamin Mendy huku Kylian Mbappe akitimkia PSG na kuishuhudia klabu hiyo kuporomoka huku ikishindwa kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ya klabu bingwa Ulaya.
AS MONACO WAELEZEA LEMAR KUTUA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment