PETR CECH KUWEKA REKODI LEO? - Darajani 1905

PETR CECH KUWEKA REKODI LEO?

Share This
Usiku wa leo kuna mchezo moja wa ligi kuu Uingereza kati ya majirani zetu wa mji mmoja, Arsenali watakaomenyana na majirani zetu wengine lakini hawa wanatoka mbali kidogo na sisi tulipo, wanatokea Meriyside, Liverpool.

Lakini katika mchezo huo kuna mtu anaweza akaweka rekodi mpya, mtu huyo ni aliyewai kuwa kipa bora kwenye dhama zake akiwa klabuni Chelsea, Petr Cech. Ambaye kama atacheza katika mchezo wa leo, na akatooka bila kufungwa basi atakuwa ameweka rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kutoruhusu kufungwa katika michezo mingi au kwa kiingereza tunasema cleansheet.

Petr Cech akifanikiwa kutokufungwa atakuwa kipa wa kwanza kucheza michezo mingi bila kufungwa ambapo rekodi hiyo ataifikia kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata Chelsea akicheza kwa misimu mingi kabla ya kutimkia Arsenal. Ambapo ameanza kuidakia Chelsea toka msimu wa 2004/2005 mpaka kuondoka msimu wa 2014/2015.
Rekodi ya Petr Cech ya kupata "cleansheets" akiwa klabuni Chelsea

No comments:

Post a Comment