CHELSEA KUPISHANA NA MANYUMBU - Darajani 1905

CHELSEA KUPISHANA NA MANYUMBU

Share This
Kampuni au mtandao wa FiveThirtyEight unaotumia fivethirtyeight.com umechapisha utabiri wake katika msimamo wa ligi kuu Uingereza jinsi utakavyoisha katika nafasi za juu.

Mtandao huo ambao hutumia takwimu katika kufanya utabiri katika mambo mbalimbali inaamini Chelsea ina nafasi kubwa ya kumaliza kama mshindi wa pili katika msimamo huo wa ligi kuu huku timu ya Manyumbu(Man utd) iliyoko nafasi ya pili kwa sasa ikipewa uwezekano wa kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu.

Chelsea kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama 39 huku ikiachwa alama tatu na Manyumbu wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 42. Huku ubingwa wa ligi hiyo ikikabidhiwa Mama site(Manchester city) inayoongoza kileleni kwa tofauti ya alama 13 dhidi ya Manyumbu.
Je unazani utabiri wao utakuwa kweli?
jinsi msimamo ulivyotabiriwa na mtandao huo wa FiveThirtyEight.com

No comments:

Post a Comment