Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anaendelea kupata lawama nyingi mara baada ya suluhu katika mchezo wa jana dhidi ya Everton, huku akilaumiwa sana kwa kumuacha nje Michy Batshuayi mpaka kuja kumwingiza dakika ya 71 ya mchezo huo.
Mchambuzi wa michezo, Jamie Redknapp naye hajasita kutoa lawama zake kwa kocha huyo.
Redknapp alisema "sijui Conte alikuwa anawaza nini kumweka Michy(Batshuayi) nje, unamweka vipi nje mshambuliaji wakati mchezo ulikuwa mgumu na unahitaji matokeo. Katika mchezo ule haukuhitaji mpira wa ufundi mwingi, ulimuitaji mtu mmoja atakayekuwa mmaliziaji na kufunga goli moja baya ambalo lingeinufaisha timu"
"Badala yake unamchelewesha mmaliziaji ambae kiasili ni mshambuliaji wa kati na unamchezesha Hazard ambae ni winga. Tushazoea Michy anakaa nje wakati ambao Alvaro(Morata) yupo ndani, lakini pale Alvaro hayupo na bado unamweka nje? sijui huwa anawaza nini Conte" alisema mchambuzi huyo.
Mwenyewe Antonio Conte alipohojiwa jana kuhusu Batshuayi alisema msimu huu ndio amecheza michezo mingi kuliko msimu uliopita lakini ata hivyo mchezaji huyo alikuwa majeruhi kabla ya kurejea muda mfupi.
No comments:
Post a Comment