KTBFFH; MFAHAMU ZAIDI AZPILICUETA - Darajani 1905

KTBFFH; MFAHAMU ZAIDI AZPILICUETA

Share This
Moja kati ya wachezaji nyota na kipenzi cha watu klabuni Chelsea ni Cesar Azpilicueta akiwa na mafanikio makubwa kikosini hapo akicheza michezo karibu yote ambayo Chelsea inashuka uwanjani ambapo kwa upande wa Ligi kuu Uingereza, Azpilicueta amecheza michezo yote chini nya kocha Antonio Conte kasoro mchezo mmoja tu.

Sasa leo nataka tukamwangalie Cesar Azpilicueta ni nani maisha yake kwa ujumla na akiwa kama mchezaji wa Chelsea.

Azpilicueta ni nani?
Cesar Azpilicueta Tanco ndiye jina lake kamili, akiwa amezaliwa tarehe 28-agosti mwaka 1989 katika jiji la Pamplona nchini Hispania. Ni mchezaji wa Chelsea huku kwa upande wa taifa akilitumikia taifa la Hispania akicheza kama mlinzi wa pembeni.


Maisha yake ya soka
Azpilicueta alinza kucheza soka katika klabu ya jijini kwao Pamplona, klabu ya Osasuna akiwa katika akademi ya klabu hiyo ambapo aliingia huko mwaka 2001 akacheza huko mpaka mwaka 2007 alipopandishwa kwenye timu ya wakubwa huku akianza kucheza kama mshambuliaji kabla ya baadae kuhamishwa namba na kucheza kama kiungo na baadae tena kuwa kama mlinzi wa kati.

Kwenye timu ya wakubwa alikaa kwa miaka mitatu tu kabla ya kuuzwa kwenda Olympique Marseille ya nchini Ufaransa ambapo kiasi cha Uero milioni 7 ndico kilitumika kumuuza nyota huyo kwenda Marseille. Aliichezea Marseille michezo 47 huku akifunga goli moja ambalo alilifungwa katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya kabla ya baadae klabu kubwa kadhaa zikaanza kumfukuzia huku Chelsea ikiongoza katika mbio hizo, hiyo ilikuwa mwaka 2012. Na ndipo rasmi Azpilicueta Tanco akajiunga na Chelsea kwa kiasi cha paundi milioni 7.

Maisha yake ndani ya Chelsea
 24-agosti-2012 ndio usajili wa Azpilicueta kujiunga na Chelsea ulikamilika kwa kiasi cha kukadiriwa kuwa ni paundi milioni 7 ambapo mara baada ya kufika Chelsea, nyota mwenzake raia wa Hispania, Juan Mata alisema "Cesar ni beki aliyekamilika, ana kasi na amejaaliwa kila kitu".

Azpilicueta alicheza katika mchezo wake wa kwanza tarehe 25-septemba-2009, alipoanza katika kikosi kilichoshinda 6-0 dhidi ya Wolves katika mchezo wa kombe la ligi na katika mchezo wa ligi kuu alicheza mchezo wake wa kwanza akiingia kama mchezaji wa akiba akichukua nafasi ya Branislav Ivanovic dhidi ya Norwich ambapo Chelsea ilishinda 4-1.

Azpilicueta alizidi kupata nafasi ya kucheza huku akiwemo katka kikosi cha kocha Rafa Benitez katika mchezo wa fainali ya kombe la Europa dhidi ya Benfica hiyo ikiwa mwaka 2013 ambapo mchezo huo ulichezwa katika jiji la Amsterdam huko nchini Uholanzi ambapo aliiongoza vyema Chelsea kutwaa taji hilo kwa magoli 2-1 huku hilo goli moja la Benfica likifungwa kwa njia ya penati iliyotokea mara baada ya Azpilicueta kushika mpira.

Azpilicueta alifunga goli lake la kwanza la kiushindani katika mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Arsenal katika mchezo ulioishuhudia Chelsea ikishinda 2-0, hiyo ilikuwa mwaka 2013.

Mara baada ya kurudi kwa kocha Jose Mourinho klabuni Chelsea kukaanza kumfanya Azpilicueta awe anapata nafasi ya kucheza zaidi katika upande wa kushoto akiwa kama mlinzi wa kushoto akichukua nafasi ya Ashley Cole. Mourinho alipohojiwa kuhusu Cesar alisema "nampenda sana Azpilicueta, nadhani kwenye timu yako ukiwa na wachezaji 11 kama Azpilicueta basi unaweza kushinda hata Uefa" ambapo katika msimu huo Azpilicueta alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa wachezaji yaani Player's Player of the Year klabuni Chelsea.

Baada ya muda kupita na matukio mengi hapo kati tunadondokea msimu wa 2016-2017, Azpilicueta akitumika katika michezo yote ya ligi kuu akiwa ndiye mchezaji pekee kufanyiwa hivyo chini ya kocha Antonio conte na hivyo kuisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu katika msimu wa kwanza tu kwa Antonio Conte kuchukua majukumu ya kuifundisha Chelsea.

Na mara baada ya mkongwe John Terry kuachana na Chelsea na kutimkia zake Aston Villa, ndipo Gary Cahill akachaguliwa kuwa nahodha wa timu huku Cesar Azpilicueta akipewa unahodha usaidizi.

Timu ya taifa
Cesar ameshachaguliwa mara kadhaa kutumikia timu yake ya taifa akiwa kama mlinzi wa pembeni akishiriki kwenye michuano kama kombe la dunia mwaka 2014 na michuano ya mabara mwaka 2013 yote yakifanyika nchini Brazil. Huku kwa soka la vijana akilitumikia taifa lake katika ngazi karibu zote akicheza katika kikosi cha Hispania chini ya miaka 16, 17, 19, 21 na 23 ambapo huko kote amecheza jumla ya michezo 84 na kufunga magoli 3.

No comments:

Post a Comment